Mtaalamu asema China iko mstari wa mbele katika kutengeneza, kutumia teksi zisizo na dereva

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 03, 2023

Gari linalojiendesha (la kwanza kulia) likiwa kwenye majaribio katika barabara ya Yizhuang ya Beijing, China, Oktoba 19, 2021. (Xinhua/Peng Ziyang)

Gari linalojiendesha (la kwanza kulia) likiwa kwenye majaribio katika barabara ya Yizhuang ya Beijing, China, Oktoba 19, 2021. (Xinhua/Peng Ziyang)

Mtaalam wa Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Usimamizi (IMD) Bw. Howard Yu amesema kuanza kutumika kwa teksi zisizo na dereva nchini China kunatazamiwa kutandika njia kwa kazi ya upangaji wa miji kwa kutumia teknolojia, kupunguza msongamano wa magari na kupunguza utoaji wa kaboni.

Bw. Howard Yu ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha IMD kuhusu utayari wa baadaye, amesema hili ni jambo ambalo limekuja kwa wakati na linalofaa, kwani teksi hizo zitaboresha usalama barabarani, ufanisi na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni, na pia itakuwa ni njia rahisi sana ya usafiri.

Mwezi Machi mwaka huu serikali ya China ilitoa leseni kwa kampuni kubwa ya teknolojia ya China ya Baidu na kampuni ya Pony.ai kwa ajili ya teksi zisizo na dereva.

Gari linalojiendesha bila dereva la kampuni ya Didi likipita barabarani katika eneo la Huadu, Guangzhou, Mkoani Guangdong kusini mwa China. Machi 27, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

Gari linalojiendesha bila dereva la kampuni ya Didi likipita barabarani katika eneo la Huadu, Guangzhou, Mkoani Guangdong kusini mwa China. Machi 27, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

Katika kipindi cha miezi minne iliyopita, jumla ya teksi 116 zinazojiendesha bila dereva zimekamilisha zaidi ya safari milioni 1.5 za majaribio, na kupata zaidi ya asilimia 95 ya maoni chanya kutoka kwa abiria. Hatua hii inaonesha kuwa kwa mara ya kwanza magari yanayojiendesha yamepewa ruhusa ya kutoa huduma katika mji mkubwa.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la ushauri la IHS Markit, thamani ya soko la teksi zinazojiendesha bila dereva nchini China linatarajiwa kufikia yuan trilioni 1.3 (sawa na dola za kimarekani bilioni 180) ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni asilimia 60 ya soko la usafiri wa teksi nchini China.

Gari linalojiendesha likiwa kwenye majaribio ya kujiendesha bila dereva kwenye barabara ya Yizhuang ya Beijing, China Oktoba 19, 2021.(Xinhua/Peng Ziyang)

Gari linalojiendesha likiwa kwenye majaribio ya kujiendesha bila dereva kwenye barabara ya Yizhuang ya Beijing, China Oktoba 19, 2021.(Xinhua/Peng Ziyang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha