Teknolojia rafiki kwa mazingira zachangia Michezo ya Dunia ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Chengdu Universiade

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2023

Picha iliyopigwa Aprili 18, 2023 ikionyesha kumbi za Eneo Maalum la Michezo la Ziwa Dong'an huko Chengdu, Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Shen Bohan)

Picha iliyopigwa Aprili 18, 2023 ikionyesha kumbi za Eneo Maalum la Michezo la Ziwa Dong'an huko Chengdu, Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Shen Bohan)

CHENGDU - Michezo ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya majira ya joto ya FISU ya Chengdu, iliyopangwa kufunguliwa Ijumaa huko Chengdu, Mji Mkuu wa Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, huu ni mfano mzuri wa maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache katika hali ya kuongezeka kwa mahitaji ya nishati ya umeme na joto kali.

Wakati huo huo, maendeleo ya China katika kuhimiza ukuaji wa uchumi bila kutoa uchafuzi mwingi kwa mazingira yataonyeshwa kikamilifu wakati wa shughuli hii ya michezo.

Michezo hiyo ya wanamichezo vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani imekumbatia teknolojia za kisasa ambazo siyo tu zitatoa uzoefu wa kuburudisha kwa washiriki wakati wa msimu wa joto lakini pia kuacha urithi wa kijani wa kudumu kwa michezo hiyo na washiriki wake.

Majira ya joto huko Chengdu ni ya joto na unyevu huku kukiwa na upepo mdogo. Ili kuweka majengo kuwa na ubaridi katikati ya mawimbi ya joto huku yakidumisha utoaji wa kaboni chache, wasanifu wamebuni vichochoro vyenye umbo la hourglass ndani ya majengo, ambavyo vinaweza kuongeza mtiririko wa hewa na hivyo kuondoa joto.

Zhong Peng, Mkuu wa Muundo wa Kijiji cha Michezo cha FISU, ametoa maelezo kuhusu "uchochoro wa baridi" aliobuni, akitoa takwimu za uokoaji mkubwa wa nishati uliopatikana kwa kubadilisha matumizi ya kiyoyozi kupitia kutumia mtiririko endelevu wa hewa.

"Mahali hapa panachukua eneo la mita za mraba 1,400. Kama kiyoyozi kingewashwa, matumizi ya nishati ya kila mwaka ya kiyoyozi yangefikia karibu 70,000 kWh, ambayo ni sawa na matumizi ya jumla ya nishati ya familia 20 kwa mwaka," Zhong amesema.

Ukiacha hatua za kupoza joto, Chuo Kikuu cha Chengdu pia kinaangazia teknolojia zenye kutoa kaboni chache, huku uzoefu wa kujiendesha wa magari yanayotumia ya nishati mpya (NEVs) ukiwa ni programu mashuhuri wa kuangazia.

Kwenye uwanja wa kufanyia mashindano ya Michezo ya jeminestik ya kisanii na mazoezi ya kabla ya mashindano katika jengo la kufanyia michezo mbalimbali kwenye Eneo Maalum la Michezo la Ziwa Dong'an, mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya nishati umewekwa ili kurekodi data za wakati halisi na kuchambua matumizi ya nishati ya vifaa katika maeneo yote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha