China yaweka rekodi ya kuzalisha magari milioni 20 yanayotumia nishati mpya (NEVs)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2023
China yaweka rekodi ya kuzalisha magari milioni 20 yanayotumia nishati mpya (NEVs)
Wafanyakazi wakiweka mikanda ya mipira kwa ajili ya kuziba milango kwenye mstari wa kuunganisha sehemu za gari katika kiwanda cha kampuni ya magari ya GAC Aion, ambayo ni kampuni tanzu ya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) ya Kampuni ya magari ya Guangzhou (GAC Group), huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Februari 24, 2023. (Xinhua/Deng Hua)

GUANGZHOU - Gari linalofanya idadi ya magari ya China yanayotumia nishati mpya (NEVs) kufika milioni 20 limeondoka kwenye mstari wa uzalishaji siku ya Jumatatu huko Guangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China na kuweka rekodi ya kihistoria kwa sekta ya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) ya nchi hiyo.

Gari hilo limezalishwa na kampuni ya kuunda magari yanayotumia nishati mpya ya GAC Aion. Kwa rekodi hii, sekta ya magari yanayotumia nishati mpya ya China imeingia katika hatua mpya ya maendeleo makubwa, ya utandawazi na ubora wa kiwango cha juu, na inakuwa sehemu muhimu ya mfumo wa kisasa wa viwanda wa China, kwa mujibu wa Fu Bingfeng, makamu mkuu mtendaji na katibu mkuu wa Shirikisho la Wazalishaji Magari la China (CAAM).

Tangazo hilo limetolewa na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China kwenye hafla ya kusherehekea rekodi hiyo mpya iliyofanyika Guangzhou.

"NEV ndiyo mwelekeo mkuu wa mabadiliko, uboreshaji na maendeleo yasiyoleta uchafuzi ya tasnia ya magari duniani, na pia ni chaguo la kimkakati kwa maendeleo yenye sifa bora ya sekta ya magari ya China," Xin Guobin, naibu waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China amesema katika hotuba yake kwenye hafla hiyo.

Katika kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, China ilikuwa imezalisha zaidi ya magari milioni 3 na kuuza magari milioni 2.94 yanayotumia nishati mpya, ikiwa ni ongezeko la asilimia 45.1 na asilimia 46.8 mtawalia kuliko mwaka jana wakati kama huo, kwa mujibu wa CAAM.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha