China yaweka mkazo katika kuongeza uzalishaji wa mazao kwenye ardhi ya chumvi na alkali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2023

Watu wakitazama sampuli za mpunga unaostahimili ardhi ya chumvi na alkali kwenye Maonyesho ya 13 ya China-Asia Kaskazini-Mashariki huko Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini-Mashariki mwa China, Septemba 24, 2021. (Xinhua/Xu Chang)

Watu wakitazama sampuli za mpunga unaostahimili ardhi ya chumvi na alkali kwenye Maonyesho ya 13 ya China na Asia Kaskazini-Mashariki huko Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini-Mashariki mwa China, Septemba 24, 2021. (Xinhua/Xu Chang)

BEIJING - Mwezi Mei, upande wa magharibi wa Mkoa wa Jilin ulioko Kaskazini-Mashariki mwa China ulianzisha msimu wa kilimo wa majira ya mchipuko, na shamba ambalo hapo awali lilikuwa lisiloweza kuzalisha mazao kwenye ardhi ya chumvi-alkali sasa linakabiliwa na ngurumo ya mashine za kilimo.

Udongo wa chumvi na alkali ni mgumu sana kulima, na hutoa mazao machache. Hata hivyo, wakulima wa eneo hilo sasa wananufaika na juhudi za kuboresha ardhi hiyo, kwa kutumia maji kuosha chumvi hiyo, hivyo kuifanya kuwa ya kufaa kwa uzalishaji wa kilimo.

Miradi mingi mikubwa ya kuhifadhi maji imetekelezwa magharibi mwa Jilin, ikipitisha mikondo ya maji kama vile Mto Nenjiang na Mto Songhua kuelekea kwenye mito na maziwa makubwa katika eneo hilo, na kutengeneza mfumo wa mtandao wa maji wa kutibu udongo.

Shen Qiang, mfanyakazi aliyezaliwa "baada ya mwaka wa 1990" katika kampuni moja ya kilimo ya eneo hilo, alikuja katika Kitongoji cha Haituo katika Mji wa Da'an Mwaka 2019. Ameshuhudia mabadiliko ya hatua kwa hatua ya ardhi ya chumvi-alkali kuwa mashamba ya mpunga.

“Tunatakiwa kumwagilia na kuondoa maji kwenye ardhi mara kadhaa ili kupunguza chumvi na alkali ya udongo ili miche ya mpunga ikue vizuri,” amesema.

Takwimu zinaonyesha kuwa China imedumisha uzalishaji wake wa mazao ya nafaka kwa mwaka kwa zaidi ya tani milioni 650 kwa miaka mfululizo, kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ya kilimo.

Katika muongo uliopita, kiwango cha mchango wa maendeleo ya sayansi ya kilimo nchini China kiliongezeka kwa asilimia 7 hadi kufikia zaidi ya asilimia 61. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha