

Lugha Nyingine
Majaribio ya teknolojia ya anga ya juu ya China yatoa matokeo yenye matunda
![]() |
Picha hii ya skrini iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya Juu cha Beijing Novemba 3, 2022 ikionyesha wanaanga wa Shenzhou-14 Chen Dong (Kati), Liu Yang (Kushoto) na Cai Xuzhe wakipunga mkono ndani ya moduli ya maabara ya Mengtian. (Picha na Sun Fengxiao/Xinhua) |
BEIJING - Kwa mara ya kwanza kabisa, China imekamilisha majaribio ya usimamizi wa joto la metali kimiminika kwenye obiti katika kituo chake cha anga ya juu cha Tiangong, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limetangaza.
Wakati wa majaribio hayo, mashine ilifanya kazi kwa utulivu, na msururu wa teknolojia muhimu za metali zenye msingi wa bismuth, kama vile kuyeyuka kwa kudhibitiwa, upanuzi na uhamishaji wa joto ulithibitishwa kwenye mazingira ya nguvu ndogo, CMSA imesema.
Tangu moduli hiyo ya maabara iliporushwa Oktoba mwaka jana, imeleta matunda yenye manufaa katika majaribio ya teknolojia ya anga ya juu, ikiwa ni pamoja na kuthibitisha hali ya metali kimiminika kwenye anga ya juu.
Sifa kadhaa zinazohitajika za metali kimiminika kama vile upitishaji bora wa umeme, kiwango cha juu cha joto la kuchemsha na uwezo mzuri wa upitishaji joto huzifanya zilete matumaini katika matumizi kwenye safari zijazo za vyombo vya anga ya juu.
Tangu chombo hicho kiingie kwenye obiti, vipimo na majaribio kadhaa yamefanyika, kupata data juu ya uhamisho wa joto wa convection wa metali kimiminika na udhibiti wa halijoto inayoleta mabadiliko ya hali ya metali hiyo katika mazingira ya nguvu ndogo (microgravity), imesema CMSA.
Hii Pia ni mara ya kwanza kwa China kufanya majaribio hayo kwenye anga ya juu, CMSA imeongeza.
Shirika hilo limeongeza kusema kuwa, kila mradi wa majaribio ya teknolojia ya anga ya juu ya China unafanywa na kuendelea vizuri kama ilivyopangwa, na matunda zaidi kutoka kwa kituo hicho cha anga ya juu yanatarajiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma