

Lugha Nyingine
China yajiandaa kurusha chombo cha anga ya juu cha Tianzhou-6
Picha hii iliyopigwa Mei 7, 2023 ikionyesha chombo cha anga ya juu cha Tianzhou-6 kikiwa pamoja na roketi ya kubeba ya Long March-7 Y7 vitakavyohamishwa katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Picha na Qiu Lijun/Xinhua)
WENCHANG, Hainan - Chombo cha anga ya juu cha Tianzhou-6 kikiwa pamoja na roketi ya kubeba ya Long March-7 Y7 vimehamishwa kiwima hadi eneo la kurusha roketi na vyombo kwenye anga ya juu siku ya Jumapili.
Chombo hicho cha anga ya juu kitarushwa siku za mbeleni kwa wakati ufaao, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China.
Shirika hilo limesema, zana na vifaa katika Sehemu ya Kurusha Vyombo kwenye Anga ya Juu ya Wenchang katika mkoa wa kisiwa wa Hainan Kusini mwa China viko katika hali nzuri, na ukaguzi mbalimbali wa kazi kabla ya urushaji na majaribio ya pamoja yatafanywa kama ilivyopangwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma