

Lugha Nyingine
China yashuhudia maendeleo katika ushirikiano wa haki miliki (IP) na nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja
Picha iliyopigwa Oktoba 27, 2021 ikionyesha lori la kwanza la China la kutoa huduma ya kutia nta kwenye ubao wa kuteleza kwenye theluji lenye hakimiliki ya kujitegemea hapa Beijing, China. (Xinhua/Chen Zhonghao)
BEIJING - China imeshuhudia maendeleo thabiti kwenye mabadilishano na ushirikiano katika haki miliki (IP) na nchi zilizo kando ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), Idara ya Kitaifa ya Hakimiliki ya China imesema Jumatatu.
Jumla ya nchi 115 za BRI ziliwasilisha maombi ya hataza 253,000 katika muongo mmoja uliopita nchini China, ikiwa na wastani wa ongezeko la kila mwaka la asilimia 5.6, Shen Changyu, Mkuu wa Idara ya Kitaifa ya Hakimiliki ya China, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Idara hiyo imetia saini mikataba ya ushirikiano na mashirika au idara za kusimamia hakimiliki za nchi 56 za BRI, na idadi ya maombi ya hataza yaliyochapishwa za kampuni za China katika nchi za BRI Mwaka 2022 ilifikia 12,000, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.4 mwaka hadi mwaka, alisema Shen.
Shen ameongeza kuwa msururu wa miradi ya ushirikiano kati ya China na nchi za BRI imetekelezwa, ikijumuisha mabadilishano ya sera za kisheria, masomo ya shahada ya uzamili na uhamasishaji wa Haki za Hakimiliki (IPR).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma