Kampuni ya Umeme wa Nyuklia ya China yatoa "Picha ya Kuchorwa ya Mwonekano wa Majenereta ya Nishati Safi ya Nyuklia”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2023

Tarehe 22, Aprili, siku ya 53 ya Sayari ya Dunia, Kampuni ya Umeme wa Nyuklia ya China (CNNP) ilitoa "Picha ya Kuchorwa ya Mwonekano wa Majenereta ya Nishati safi ya Nyuklia". “Picha hii inaonesha mchango wa CNNP katika kujenga mazingira mazuri ya asili 'kwa kutumia vyema nishati ya nyuklia kuwezesha maisha bora'.” Mhusika wa CNNP amejulisha kuwa, hadi sasa, CNNP kwa jumla imezalisha umeme wenye nguvu za kilowati trilioni 1.2 kwa saa kwa ajili ya biashara, ambao ni sawa na matokeo ya kupunguza matumizi ya makaa ya mawe sanifu kwa tani milioni 360, au kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni kwa tani milioni 9.5, au kupanda miti yenye kuenea eneo la hekta milioni 3.28.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha