

Lugha Nyingine
Chapa za teknolojia za Kichina zapata umaarufu mkubwa nchini Malawi
Bango la tangazo la chapa ya simu za mkononi ya China ya Tecno likionekana kwenye duka la simu za mkononi huko Blantyre, Malawi, Tarehe 19 Aprili 2023. (Picha na Joseph Mizere/Xinhua)
BLANTYRE, Malawi - Chapa za simu mkononi kutoka China zimepata umaarufu mkubwa nchini Malawi kutokana bei zake nafuu za watu kuweza kumudu na kutegemewa, na kutoa programu za simu zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei ya ushindani.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi majuzi zilizokusanywa na Statcounter, ambayo ni tovuti ya takwimu inayoaminika, chapa maarufu za Kichina kama vile Tecno, itel, Xiaomi, na Huawei zinachukua asilimia 59.57 ya soko nchini Malawi, ikiashiria ongezeko la ushawishi wa teknolojia ya China kwenye soko la Malawi.
Kuongezeka kwa umaarufu wa chapa za Kichina nchini humo pia kwa ujumla kumeshuhudiwa kwenye maduka mbalimbali ya teknolojia katika miji ya Malawi, ikiwa ni pamoja na Blantyre, ambapo mahitaji ya simu za mkononi daima ni makubwa.
Alfred Khonje, mwakilishi wa mauzo katika Kampuni ya Timeline Electronics katika jiji la kibiashara la Blantyre, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano kuwa simu za mkononi za China zinakidhi mahitaji ya bidhaa zenye ubora wa juu kwa bei nafuu, na kuzifanya ziweze kununulika kwa wateja wake wengi.
“Kwa wastani simu hizi zinauzwa dola za kimarekani 120 ambayo ni bei nzuri kwa mtu wa kawaida, katika kizazi cha sasa hakuna anayependa kuachwa nyuma, kuanzia kijana hadi mzee kila mtu anatamani kumiliki simu janja hali ambayo imesababisha kuongezeka kwa mahitaji, na simu hizi za China zinatoa suluhisho kubwa," Khonje amesema.
Chapa hizo pia zinafaa kwa wanafunzi kama vile Patson Kuwelenga, anayesoma katika Chuo cha Ufundi cha Soche huko Blantyre na ambaye chapa yake anayoipenda zaidi ni Xiaomi.
"Simu za Xiaomi ni zenye kuleta mageuzi kwangu; Ninazipendekeza sana kwa mtu yeyote ambaye anataka kufurahia uzoefu mpya wa teknolojia," Kuwelengeza amesema.
Wateja mbalimbali nchini Malawi, wakiwemo wanafunzi na wataalamu vijana, wamezidi kugeukia chapa za Kichina kwa mahitaji yao ya kiteknolojia, jambo linaloonyesha umaarufu unaokua na mvuto mkubwa wa bidhaa hizi nchini humo.
Wateja wakitembelea duka la simu janja huko Blantyre, Malawi, Tarehe 19 Aprili 2023. (Picha na Joseph Mizere/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma