Mkuu wa Shirika la Umeme wa Nyuklia la China: Umeme wa Nyuklia wa China waendelea kwa usalama na utaratibu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2023

 Picha hii ikionesha majenereta ya 5 na 6 ya Kituo cha Fuqing cha  Hualong One, ambacho ni mradi wa Kielelezo Duniani cha uzalishaji wa umeme kwa Nishati ya Nyuklia

Picha hii ikionesha majenereta ya 5 na 6 ya Kituo cha Fuqing cha Hualong One, ambacho ni mradi wa Kielelezo Duniani cha uzalishaji wa umeme kwa Nishati ya Nyuklia. (Picha/Xinhua)

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Kampuni ya Umeme wa Nyuklia ya China Lu Tiezhong hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Gazeti la Global Times amesema kuwa, majenereta ya umeme wa nyuklia ya China yameweka rekodi ya kuendeshwa kwa usalama na utaratibu duniani.

Hivi sasa, katika sehemu mbalimbali nchini China kuna majenereta 77 ya umeme wa nyuklia yanayofanya kazi au yanayoendelea kujengwa. Katika orodha ya viwango vya jumla vya majenereta ya umeme wa nyuklia duniani iliyotolewa na Shirikisho la Waendeshaji wa Uzalishaji wa Umeme wa Nyuklia Duniani (WANO), China imechukua nafasi ya mbele. Mnamo Mwaka 2022, majenereta ya umeme wa nyuklia ya China kwa jumla yamezalisha umeme wenye nguvu ya kilowati bilioni 417.78 kwa saa, ukichukua asilimia 4.98 ya ujumla ya umeme wote uliozalishwa nchini China mwaka huo.

“Umeme wa nyuklia ni nishati safi ya usalama, yenye ufanisi mkubwa, tulivu inayoweza kutumika katika sehemu nyingi mbalimbali,” amesema Lu.

Lu amesema kuwa, kwa kuchukua mfano wa majenereta ya Hualong No.1, yanazalisha umeme wa nyuklia karibu Kilowati bilioni 10 kwa saa kila mwaka, ambao unaweza kukidhi mahitaji ya watu milioni 1 katika nchi zilizoendelea zenye uchumi wenye ukubwa wa kati, kiwango ambacho ni sawa na kupunguza utoaji wa kaboni kwa tani milioni 8.16, pia ni sawa na ufanisi wa kupanda miti milioni 70. Tangu Kituo cha uzalishaji wa umeme kwa nishati ya nyuklia cha Qinshan, ambacho ni cha kwanza kilichokamilika nchini China Mwaka 1991, uzalishaji wa jumla wa umeme kwa nishati ya nyuklia umezidi kilowati trilioni 3.3 kwa saa, ambayo ni sawa na kupunguza utoaji wa kaboni kwa zaidi ya tani bilioni 2.4.

Lu amesema, nishati ya nyuklia inapanuka hatua kwa hatua na kurutubishwa katika nyanja za matumizi ya jumla, na inatazamiwa kuwa ufumbuzi wa matatizo ya nishati ya binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha