Ujenzi wa Nyuklia wa China: Kutoka kuwa mfuataji  wa nyuma duniani hadi kukimbia bega kwa bega, ikijipanga kuongoza katika siku zijazo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2023

Katika picha ni kinu cha kwanza duniani cha nishati ya nyuklia cha Hualong One – Kitengo cha 5 cha Mashine za Nishati ya Nyuklia  za Fujian Fuqing. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Katika picha ni kinu cha kwanza duniani cha nishati ya nyuklia cha Hualong One – Kitengo cha 5 cha Mashine za Nishati ya Nyuklia za Fujian Fuqing. (Picha imetolewa na mhojiwa)

"Kutoka kuwa 'mfuataji wa nyuma' katika siku za zamani hadi 'kukimbia bega kwa bega' leo, bila shaka 'tutaongoza' kwenye ujenzi wa nishati ya nyuklia duniani." Chen Baozhi, Mwenyekiti wa Shirika la Ujenzi wa Nyuklia la China amesema huku akieleza kuwa kauli hii siyo tu katika kujiamini kusikokuwa na uhakika, lakini pia kauli ya dhati baada ya miaka 32 ya mapambano.

"Nina heshima ya kushuhudia na kushiriki katika mchakato mzima wa uanzishwaji, maendeleo na ukuaji wa sekta ya nyuklia ya nchi yangu. Kuanzia kukamilika kwa Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Qinshan ambacho kimepata mafanikio ya kuwa mwanzilishi rasmi wa nishati ya nyuklia ya China Bara, hadi ujenzi wa vinu vya kawaida duniani vya nishati ya nyuklia kama vile Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Daya Bay, Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Tianwan, na Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Fuqing, kisha Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha kizazi cha tatu cha 'Hualong One' kilichoundwa kwa kujitegemea na nchi yetu kama 'turufu ya biashara ya kitaifa' inayong'aa duniani... ninahisi kuheshimiwa sana katika safari hii." Chen Baozhi amesema.

Tarehe 27 Novemba 2020, Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Fuqing Kitengo cha 5, ambacho ni kinu cha kwanza duniani cha Hualong One, kiliunganishwa kwenye gridi ya taifa kwa ajili ya kuzalisha umeme, na hivyo kuashiria kwamba China imevunja ukiritimba wa teknolojia ya kigeni ya nishati ya nyuklia na kuingia rasmi katika orodha ya nchi zilizo na teknolojia ya hali ya juu ya nishati ya nyuklia.

Gao Jinzhu, Naibu Meneja Mkuu wa Shirika la Ujenzi wa Nyuklia la China, ameanza kwa kusema kwamba kuna msemo wa kimataifa kwamba "kinu cha kwanza lazima kicheleweshwe". Kinu cha kwanza cha nishati ya nyuklia kawaida huhusiana na kitengo cha kwanza cha nishati ya nyuklia kinachoundwa kwa teknolojia mpya ya nishati ya nyuklia.

Kutokana na muundo wa teknolojia mpya na vifaa vipya, idadi kubwa ya matatizo huwa wazi wakati wa mchakato wa ujenzi, na uboreshaji endelevu unaohitajika wakati wa ujenzi, mara nyingi husababisha kuchelewa kwa muda wa ujenzi. Kwa mfano, muda wa ujenzi wa vinu vya kwanza vya nyuklia vya kizazi cha tatu nchini Marekani na Ufaransa umecheleweshwa kwa miaka kadhaa. Kinu cha kwanza cha Hualong No. 1 kiliunganishwa kwenye gridi ya taifa ya China na kukamilisha lengo la ujenzi kama ilivyoratibiwa, na kuwa kinu cha kwanza cha nishati ya nyuklia cha kizazi cha tatu duniani ambacho kilianza kutumika kwa muda uliopangwa.

Kwa kuwa uwezo na viwango vya vinu vya nishati ya nyuklia vya China vinavyojenga vimevuka vile vya Dunia. Ujenzi wa Nyuklia wa China umekua na kuwa biashara ya uhandisi wa nishati ya nyuklia yenye sifa kubwa ndani na nje ya nchi. Uwezo wa ujenzi wa nishati ya nyuklia umeongezwa kutoka vitengo 2 tu mwanzoni hadi kufikia 40.

Chen Baozhi anasema kuwa Shirika la Ujenzi wa Nyuklia la China limeshiriki katika ujenzi wa vinu vyote vya nyuklia ambavyo vimejengwa na vinavyoendelea kujengwa nchini humo. Kwa sasa, limejenga jumla ya vitengo 83 vya nguvu ya nyuklia, ambapo 60 kati yake tayari vimeanza kufanya kazi na 23 vinaendelea kujengwa.

“Ni nguvu kubwa kabisa ya ujenzi wa nishati ya nyuklia ya nchi yangu” amesema Chen.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha