Majaribio ya "Jua bandia" la China yafikia mafanikio na hatua muhimu kuelekea kinu cha kutoa nishati mseto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2023

Wafanyakazi wakifanya majaribio ya kuinua daraja la juu zaidi  la mkondo thabiti wa nishati wa tokamak (EAST) katika Taasisi ya Sayansi ya Fizikia ya Hefei chini ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS) Aprili 13, 2021.(Xinhua/Liu Junxi)

Wafanyakazi wakifanya majaribio ya kuinua daraja la juu zaidi la mkondo thabiti wa nishati wa tokamak (EAST) katika Taasisi ya Sayansi ya Fizikia ya Hefei chini ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS) Aprili 13, 2021.(Xinhua/Liu Junxi)

HEFEI – Majaribio ya kuinua daraja la juu zaidi la mkondo thabiti wa nishati wa tokamak (EAST), au "jua bandia" ("jua linaloundwa na binadamu") la China, yamepata operesheni thabiti ya hali ya juu ya kizuizi cha plasma kwa sekunde 403 siku ya Jumatano, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea maendeleo ya kinu cha kutoa nishati mseto.

Ufanisi huo, uliopatikana baada ya zaidi ya milipuko 120,000, umeboresha sana rekodi ya awali ya Dunia ya sekunde 101, ambayo iliwekwa na EAST Mwaka 2017.

Lengo kuu la Mfumo wa EAST, ulio katika Taasisi ya Fizikia ya Plasma chini ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (ASIPP) huko Hefei, ni kuunda muunganisho wa nyuklia kama jua, kwa kutumia vitu vinavyopatikana kwa wingi baharini ili kutoa mkondo thabiti wa nishati safi.

Song Yuntao, Mkurugenzi wa ASIPP, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano maalum kwamba umuhimu mkubwa wa mafanikio hayo upo katika hali ya muundo wa kufungwa.

Amesema, joto na msongamano wa chembe vimeongezeka sana wakati wa operesheni hiyo ya plasma ya kizuizi kikubwa, ambayo itaweka msingi thabiti wa kuboresha ufanisi wa uzalishaji wa umeme wa mitambo ya baadaye ya kuunganisha nishati na kupunguza gharama.

Tangu kuanza kufanya kazi Mwaka 2006, Mfumo huo wa EAST uliobuniwa na kuendelezwa nchini China umekuwa jukwaa la majaribio la wanasayansi wa China na kimataifa kufanya majaribio na utafiti unaohusiana na mseto wa nishati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha