

Lugha Nyingine
Huawei yapongezwa kwa kuongeza kasi ya elimu ya kidijitali nchini Ethiopia
Kampuni kubwa ya mawasiliano ya China Huawei imepongezwa kwa nafasi yake katika kuongeza kasi ya elimu ya kidijitali nchini Ethiopia.
Pongezi hizo zimetolewa kwenye mkutano wa elimu ulioandaliwa na Kampuni ya Huawezi nchini Ethiopia uliofanyika mjini Addis Ababa, chini ya kaulimbiu ya “Kuongeza Kasi ya Safari ya Elimu ya Kidijitali kwa Ethiopia.”
Akizungumza kwenye mkutano huo, mkuu wa kitengo cha TEHAMA na elimu ya kidijitali katika Wizara ya Elimu nchini Ethiopia, Zelalem Assefa amesema, nchi hiyo inaendeleza mkakati wa elimu ya kidijitali ili kuifanya elimu kupatikana kwa urahisi zaidi na shirikishi kupitia teknolojia ya kidijitali.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei nchini Ethiopia, Liu Jifan amesema, kampuni hiyo inashirikiana na wateja wake katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya elimu nchini Ethiopia, ili kuboresha sekta ya kidijitali katika nchi hiyo.
Kampuni ya Huawei, kwa kutumia teknolojia za TEHAMA, inaiunga mkono Ethiopia katika kuendeleza vipaji, kupunguza pengo katika kujifunza, na kuwezesha mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma