

Lugha Nyingine
Wanasayansi wa China watengeneza ngozi ya kielektroniki ili kuzipa roboti hisia za kuguswa
Picha hii iliyopigwa Tarehe 17 Novemba 2022 ikionyesha roboti yenye miguu minne inayotumika kukagua viwanda kwenye Maonyesho ya 5 ya Kimataifa ya Sauti ya Dunia huko Hefei, Mkoa wa Anhui nchini China. (Xinhua/Zhang Duan)
NANJING - Watafiti wa China wameunda aina mpya ya ngozi ya kielektroniki (e-skin), inayowezesha roboti kuabiri mazingira yao kupitia njia ya kugusa gizani wakati uwezo wa kuona ni mdogo.
Ngozi hiyo ya kielektroniki ya jeli ina mwonekano unaofanana na mkanda na inaiga sifa za ngozi ya binadamu, ikiwa na uwezo kama vile kunyooka na uwezo wa kujiponya. Pia ina uwezo wa kugundua mabadiliko ya halijoto na shinikizo, ikiboresha zaidi ufanisi wake kwa matumizi ya roboti.
Ugumu mkubwa katika utengenezaji wa ngozi ya elektroniki kwa muda mrefu umekuwa katika ukosefu wa raslimali zinazofaa zenye sifa za kifizikia na hisia kama ngozi ya binadamu. Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kusini-Mashariki cha China wamepata ufumbuzi kwa kutengeneza ngozi hii mpya ya kielektroniki kwa kutumia hariri asilia na raslimali zenye protini.
Pia waliongeza ayoni za kalsiamu zinazovutia maji, ayoni za hidrojeni zenye tindikali dhaifu, na nanomaterials zenye sura mbili zinazoguswa na kichocheo cha mazingira ili kusanifu ngozi ya kielektroniki.
“Ngozi hiyo ina sifa zote za kemikali za kimwili zinazofanana na ngozi halisi, kama vile kujinyoosha, uwezo wa kujiponya, asidi hafifu na shughuli za kudhibiti bakteria, na huhisi halijoto iliyopo, shinikizo na unyevunyevu mara tu zinapowashwa,” amesema Duan Shengshun, mtaalam wa timu hiyo ya utafiti.
"Ngozi ya kielektroniki ina uwezo wa kupona yenyewe," Duan ameongeza, huku akibainisha kuwa kipandikizi cha ngozi kinaweza kufanywa kwa urahisi kwa kuambatanisha kipande kipya kwenye kipande kilichokwaruzwa.
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la ACS Nano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma