Kampuni ya Huawei yafanya maonyesho ya teknolojia ya habari nchini Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2023

Watembeleaji wa maonyesho wakionekana kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu la Huawei huko Gaborone, Botswana, Machi 31, 2023. Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Watembeleaji wa maonyesho wakionekana kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu la Huawei huko Gaborone, Botswana, Machi 31, 2023. (Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei imefanya mkutano wake wa kwanza wa Mawasiliano ya Simu nchini Botswana kuanzia Jumanne hadi Ijumaa, na kuzindua suluhu za mtandao na kituo cha data.

Mkutano huo wa siku nne umevutia washiriki zaidi ya 400 kutoka serikalini, waendeshaji mawasiliano ya simu, kampuni za biashara na vyuo vikuu ili kupata uzoefu wa teknolojia na suluhu za hivi punde za sekta ya teknolojia ya habari.

Thulagano Segokgo, Waziri wa Mawasiliano, Maarifa na Teknolojia wa Botswana, ametoa shukrani kwa Huawei kwa kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kitaifa ya kidijitali ya Botswana wakati wa mkutano huo na kuhimiza kampuni hiyo kuleta teknolojia za kisasa zaidi za kivumbuzi nchini Botswana.

“Kwa miaka mingi, Huawei imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kupanga na kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) nchini Botswana ili kusaidia ujenzi wa mawasiliano ya kila mahali na sekta ya TEHAMA nchini Botswana,” amesema David Zhang, Mkurugenzi Mkuu wa Huawei nchini Botswana.

"Tunatumai kuipa Botswana uzoefu wa hali ya juu wa Teknolojia ya 5G na suluhu za mageuzi za kidijitali," amesema Zhang.

Kwenye mkutano huo, Huawei ilifanya kongamano juu ya mada isemayo "TEHAMA kwa Maendeleo ya Vijana na Ajira" kwa lengo la kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Botswana kupitia ukuzaji wa talanta.

Amesema, tangu Mwaka 2019, Huawei imetoa mafunzo ya TEHAMA kwa zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu vya Botswana kupitia programu za Mbegu kwa Wakati Ujao (Seeds for the Future) na Mafunzo ya TEHAMA ya Huawei.

“Katika siku zijazo, Huawei inapanga kutoa mafunzo ya mawasiliano kwa wanafunzi 100 wa Botswana kila mwaka,” amesema.

Puntsho Pusoetsile, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Maarifa na Teknolojia, amekaribisha mpango huo na kuhimiza kampuni zaidi kushiriki katika ukuzaji vipaji vya mawasiliano kwa wenyeji. 

Mtembeleaji wa maonyesho akijaribu vifaa vya Uhalisia Pepe kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu la Huawei huko Gaborone, Botswana, Machi 31, 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Mtembeleaji wa maonyesho akijaribu vifaa vya Uhalisia Pepe kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu la Huawei huko Gaborone, Botswana, Machi 31, 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha