Maonyesho ya Kimataifa ya Sekta ya Data Kubwa kufanyika Mei huko Guizhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2023

Picha ikionyesha mkutano na waandishi wa habari kuhusu Maonyesho ya Kimataifa ya Sekta ya Data Kubwa ya China 2023. (Picha kwa hisani ya Kamati Tendaji ya Maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Data Kubwa ya China)

Maonyesho ya Kimataifa ya Sekta ya Data Kubwa ya China 2023 yatafanyika kuanzia Tarehe 26 hadi 28, Mei huko Guiyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Guizhou Kusini-Magharibi mwa China, kwa mujibu wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo uliofanyika Beijing Februari 20.

Kaulimbiu ya maonyesho hayo ya mwaka huu ni "Kufungamana kwa Uchumi wa Kidijitali na Halisi, Kufungua siku za baadaye kwa Nguvu ya Kompyuta".

Maonyesho hayo yatajumuisha hafla ya ufunguzi na kufunga, midahalo ya hali ya juu, majukwaa ya mijadala, maonyesho ya nje ya mtandao kuhusu teknolojia mpya, bidhaa, suluhisho na matumizi katika sekta ya data kubwa, kutolewa kwa ripoti ya mafanikio makubwa ya data kubwa, mashindano na shughuli za kutangaza uwekezaji.

Maonyesho hayo yamekuwa yakifanyika Guiyang kuanzia Mwaka 2015 na yamekuwa jukwaa la kimataifa la kuonyesha mafanikio ya China katika maendeleo ya data kubwa na mkusanyiko wa rasilimali za data kubwa duniani.

Eneo Jipya la Gui'an huko Guiyang ni eneo la msingi la eneo la majaribio la kitaifa la data kubwa la China na eneo lenye idadi kubwa ya vituo vya data kubwa zaidi duniani.

Maonesho ya Viwanda ya Guiyang pia yatafanyika ili kukuza ujumuishaji wa kina wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha