Kampuni ya Huawei yaharakisha uwezo wa kidijitali katika taasisi ya mafunzo kwa wasichana nchini Kenya

(CRI Online) Februari 21, 2023

Kampuni ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya China Huawei imesema itaimarisha elimu ya kompyuta na mafunzo ya uwezo wa kidijitali katika shule za sekondari ya juu na taasisi za elimu ya juu kwa wasichana nchini Kenya.

Mkurugenzi wa wanawake na teknolojia wa kampuni ya Huawei tawi la Kenya Bibi Maureen Mwaniki, amesema Huawei imeshirikiana na chuo kikuu cha Karatina na shule ya sekondari ya juu ya St. Faustine Kerugoya iliyoko katikati ya Kenya, kwa kutoa mafunzo ya siku tatu ya uwezo wa kidijitali kupitia Akademia ya TEHAMA ya Huawei.

Bibi Mwaniki amesema uamuzi wa kuwekeza katika mafunzo ya wanawake unatokana na pengo lililoko kwa muda mrefu kwenye mafunzo ya uwezo wa kutumia kompyuta, licha ya mafanikio yaliyopatikana hivi karibuni katika kuwasajili wanawake wapatao elfu tatu kwenye ajira za TEHAMA.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha