

Lugha Nyingine
Mkoa wa Guizhou nchini China wawekeza Yuan bilioni 20 kwenye miradi ya Data Kubwa
Mfanyakazi akifanya kazi kwenye Maabara Muhimu ya Nchi ya Data Kubwa za Umma katika Chuo Kikuu cha Guizhou kilichoko Mji wa Guiyang, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Mei 27, 2022. (Xinhua/Ou Dongqu)
GUIYANG - Mkoa wa Guizhou, ambao ni kituo kikuu cha data cha Kusini-Magharibi mwa China, umetangaza Jumatatu kuwa utawekeza Yuan bilioni 20 (kama dola bilioni 2.9 za Kimarekani) katika miradi mikubwa inayohusiana na data kubwa Mwaka 2023.
Mkutano wa data kubwa wa mkoa huo uliofanyika Jumatatu ulisema kuwa, mwaka huu, Mkoa wa Guizhou unapanga kuanzisha miradi zaidi ya 200 ya uchumi wa kidijitali yenye ukuaji mkubwa.
Kwenye mkutano huo Jing Yaping, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Data Kubwa ya mkoa huo ameeleza kuwa, mkoa huo utaharakisha mpangilio wa vituo vya data, mitandao ya kompyuta, 5G na miundombinu mingine ya kizazi kijacho ya kidijitali.
Kwa mujibu wa mpango huo, kufikia Mwaka 2025, kutakuwa na vituo 800,000 vya data kubwa na seva milioni 4 huko Guizhou, na zaidi ya vituo 180,000 vya msingi vya 5G vikiwa vimejengwa katika mkoa huo.
Mkoa wa Guizhou ukiwa ni eneo la kwanza la kitaifa la majaribio ya pande zote ya data kubwa, umekuwa ukikuza sekta ya data kubwa kama mhimili mkuu wa maendeleo yake ya kiwango cha juu ya kijamii na kiuchumi.
Mnamo Mwaka 2023, Pato la Jumla la Guizhou (GDP) linatarajiwa kuongezeka kwa karibu asilimia 6 hadi kufikia yuan trilioni 2.2, huku uchumi wa kidijitali ukichukua karibu asilimia 40 ya pato hilo la jumla.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma