Watafiti wa China wabuni mbinu za kupima haraka virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Monkepox

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2022

BEIJING - Baadhi ya watafiti kutoka China hivi karibuni wamebuni mbinu tatu za upimaji wa haraka wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Monkepox (MPXV) ambazo zinaweza kutoa matokeo ndani ya dakika 20 hadi 30 na zina kasi zaidi kuliko kipimo cha wakati halisi cha polymerase chain reaction (PCR) kinachotumika sasa.

Kipimo cha wakati halisi cha PCR kwa sasa ndicho kiwango muhimu zaidi cha upimaji wa MPXV, lakini kinahitaji wafanyakazi wa maabara waliofunzwa na vifaa maalum, na matokeo yanaweza kupatikana tu baada ya saa kadhaa.

Watafiti kutoka Taasisi ya Pasteur ya Shanghai chini ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China wameandika Makala tatu za kitafiti kuhusu majaribio ya ukuzaji wa isothermal kwa kutumia recombinase kwa ugunduzi wa haraka wa MPXV na waligundua kuwa matokeo ya jaribio yalilingana na kipimo cha wakati halisi cha CR kinachotumika sasa.

Mbinu mpya za upimaji zilikuwa zikionesha mwitikio dhidi ya MPXV pekee na mwitikio usiovuka malengo ya upimaji dhidi ya virusi vingine vya tetekuwanga, kama vile virusi vya vaccinia, na matokeo yanaweza kuonekana baada ya dakika 20 hadi 30, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti yaliyochapishwa katika jarida la Virusi.

Kwa mujibu wa utafiti huo, matokeo haya yanatoa chaguo jipya kwa utambuzi wa mapema wa kesi zinazoshukiwa za MPXV, na yatasaidia kudhibiti na kuzuia milipuko ya sasa na inayowezekana ya siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha