Shanghai yaanza kutoa chanjo ya kuvutwa dhidi ya Korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2022

Mkazi akivuta chanjo ya nyongeza ya kuvutwa dhidi ya UVIKO-19 Jumatano ya wiki hii kwenye Hospitali ya Zhongshan ya eneo la Changning, Shanghai, China. (Picha inatoka ChinaDaily)

Shanghai ilianza kutoa chanjo tamu dhidi ya korona bila ya sindano kuanzia Jumatano ya wiki hii, na watu wanaoogopa sindano au kupendelea urahisi wamekwenda kuchanjwa chanjo ya aina hiyo.

“Hii ni mchakato rahisi sana,” alisema Bw. Ma Haitao, ambaye aliagiza kwenye mtandao wa intaneti na kwenda mpaka Hospitali ya Tianshan ya Shanghai kuchanjwa chanjo ya aina hiyo Jumatano ya wiki hii.

Chanjo hiyo inawekwa ndani ya kikombe. Wachanjwa wanavuta hewa kwa nguvu kutoka kikombe, kusita kupumua kwa sekundi 5 hivi, halafu wakapumua polepole.

“Chanjo hii ni kitamu kidogo,” alisema Ma Haitao.

Shanghai Jumanne ilitangaza kuwa, itatoa chanjo ya kuvutwa dhidi ya UVIKO-19 ya kampuni ya CanSino Biologics kama chanjo ya nyongeza, ikiifanya kampuni hiyo iwe kampuni ya kwanza ya kutoa chanjo ya kuvutwa dhidi ya UVIKO-19 nchini China. Chanjo ya aina hiyo imeidhinishwa na Mamlaka ya Ukaguzi na Usimamizi wa Dawa ya China mapema ya Septemba.

Madaktari wa hospitali walisema, hospitali ya Tianshan ilianza kutoa chanjo saa 2:30 Jumatano asubuhi, na watu 30 walichanjwa na chanjo ya aina hiyo asubuhi ya siku hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha