Kituo cha unajimu cha kufuatilia Jua cha China kimeanzishwa kwenye anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2022

Roketi ya Changzheng No.2 D kilichobeba Kituo cha kufuatilia Jua cha China kwenye anga ya juu (ASO-S) ikirushwa kutoka Kituo cha kurusha roketi cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China tarehe 9, Oktoba, 2022. (Xinhua/Wang Jiangbo)

Kituo cha unajimu cha kufuatilia Jua cha China kwenye anga ya juu (ASO-S) kilichobebwa na roketi iliyorushwa ya Changzheng No.2 D kilifaulu kuingia kwenye obiti iliyopangwa tarehe 9, Oktoba saa 1:43 asubuhi kwa saa za Beijing.

Katika hekaya ya China, kuna hadithi iliyosimulia jitu jasiri Kuafu aliyeshikilia kukimbiza Jua bila kusita, hivyo kituo hiki cha unajimu kina jina la utani liitwalo “Kuafu-1”. Kituo hicho kitafanya kazi kwa zaidi ya asilimia 96 ya muda wa mwaka mzima.

Baada ya majaribio ya miezi 4 hadi 6, satelaiti hiyo yenye uzito wa kilogramu 859 kitaanza kufanya kazi ya kawaida ya kuchunguza hali ya kisayansi ya Jua kwenye umbali wa kilomita 720 kutoka ardhi ya Dunia, ili kutoa takwimu za kuunga mkono utabiri wa hali ya hewa kwenye anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha