

Lugha Nyingine
NASA na SpaceX zarusha chombo cha wanaanga kwenye kituo cha kimataifa cha anga ya juu
![]() |
Roketi ya SpaceX Falcon 9 iliyobeba Chombo cha Anga ya Juu cha Dragon Endurance ikirushwa kwenye chombo cha NASA cha SpaceX Crew-5 kwenda Kituo cha Kimataifa cha Anga ya juu (ISS) katika Kituo cha Anga cha NASA cha Kennedy huko Florida, Marekani, Oktoba 5, 2022. Idara ya Taifa ya Anga ya juu ya Marekani (NASA) na SpaceX kwa pamoja zimerusha roketi iliyobeba wanaanga wa chombo cha Crew-5 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga ya Juu (ISS) siku ya Jumatano. (Joel Kowsky/NASA/Kutumwa kupitia Xinhua) |
LOS ANGELES - Idara ya Taifa ya Anga ya juu ya Marekani (NASA) na SpaceX kwa pamoja zimerusha roketi iliyobeba wanaanga wa chombo cha Crew-5 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga ya Juu (ISS) siku ya Jumatano.
Roketi hiyo ya SpaceX Falcon 9 na Chombo cha Anga ya Juu cha Dragon Endurance vilirushwa kutoka kwenye Eneo la Urushaji vyombo kwenye anga ya juu cha 39A katika Kituo cha Anga cha NASA cha Kennedy huko Florida saa sita mchana kwa saa za Amerika Mashariki.
Muda mfupi baada ya kurushwa kwa chombo hicho, NASA ilithibitisha kukatwa kwa injini kuu na mgawanyiko wa hatua.
Hatua ya kwanza ya roketi ya Falcon 9 ilikamilisha kushuka na kutua kwa mafanikio kwenye chombo cha SpaceX, karibu na pwani ya Florida.
Chombo cha anga ya juu cha Dragon Endurance kimejitenga na hatua ya pili, na kuelekea kituo cha kimataifa cha anga ya juu (ISS).
Misheni hiyo ya anga ya juu inahusisha kuwabeba wanaanga wa NASA Nicole Mann na Josh Cassada, pamoja na mwanaanga wa Shirika la Utafiti wa Anga ya Juu la Japan Koichi Wakata, na mwanaanga wa Roscosmos Anna Kikina kuelekea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga ya juu (ISS).
NASA imesema wanaanga hao wamefika salama kwenye obiti. Chombo hicho kitatia nanga kwenye kituo cha anga ya juu takriban saa 10:57 Saa za Mashariki siku ya Alhamisi.
Kwa mujibu wa SpaceX, wakati wa muda wao kwenye maabara inayozunguka, wanaanga hao watafanya zaidi ya majaribio 200 ya sayansi na maonyesho ya teknolojia katika maeneo kama vile afya ya binadamu na mifumo ya mafuta ya mwezi.
Baada ya chombo hicho kutia nanga kwenye maabara inayozunguka, wanaanga wengine wanne wa kituo, wa misheni ya Crew-4, watamaliza misheni yao na kurejea Duniani zaidi ya wiki moja baadaye, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NASA.
Wanaanga wa Crew-4 wataondoka kituo cha anga ya juu na kutua kwenye pwani ya Florida.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma