China yachaguliwa tena kama mjumbe wa baraza la ITU

(CRI Online) Oktoba 06, 2022

China Jumatatu ilichaguliwa tena kuwa mjumbe wa baraza la Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Simu (ITU), shirika maalumu la Umoja wa Mataifa. Wakati huohuo, mkurugenzi wa Kituo cha Kufuatilia Redio ya Taifa cha China Cheng Jianjun amechaguliwa kama mjumbe mpya wa Bodi ya Udhibiti wa Redio ya ITU kwa miaka minne.

Mkutano wa Wajumbe wa ITU (PP-22) ulifunguliwa Septemba 26 huko Bucharest, na umepangwa kuendelea hadi Oktoba 14. Kiongozi wa Ujumbe wa China ambaye ni Naibu Waziri wa Teknolojia ya Viwanda na Habari Zhang Yunming alitoa hotuba na kusema kwamba China inazingatia falsafa ya maendeleo ya watu na inahimiza kikamilifu maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano pamoja na miundombinu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha