

Lugha Nyingine
Wanaanga wa China walioko kwenye safari ya chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 watoka nje ya kituo cha anga cha China
Picha ya skrini iliyopigwa kwenye Kituo cha udhibiti wa safari kwenye anga ya juu cha Beijing ikionesha kuwa, mwanaanga wa Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 Chen Dong akifunga mlango wa moduli ya maabara ya Wentian ya kituo cha anga ya juu baada ya shughuli ya kutoka nje ya chombo kukamilika tarehe 2, Septemba, 2022. (Picha/Xinhua)
Wanaanga wa China walioko kwenye safari ya chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 wametoka nje ya kituo cha anga ya juu cha China leo tarehe mosi Septemba kwa mara ya kwanza tangu wawasili kituoni humo mwezi Juni mwaka huu.
Saa kumi na mbili na dakika 26 leo jioni kwa saa za Beijng, mwanaanga Chen Dong alifungua mlango wa kutoka nje wa moduli ya maabara ya Wentian na saa moja na dakika 9 jioni akafanikiwa kutoka nje ya kituo hicho pamoja na mwenzake Liu Yang huku mwanaanga mwingine Cai Xuzhe akifanya kazi ndani ya kituo kuwasaidia wenzake pale nje.
Picha ya skrini iliyopigwa kwenye kituo cha udhibiti wa safari kwenye anga ya juu cha Beijing ikionesha kuwa, wanaanga wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 Chen Dong (kulia) na Liu Yang wakifanya shughuli ya kutoka nje ya chombo cha moduli ya maabara ya Wentian ya kituo cha anga ya juu tarehe mosi, Septemba, 2022. (Picha/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma