

Lugha Nyingine
Ukuaji wa mimea katika maabara ya anga ya juu ya China uko katika hali nzuri
![]() |
Picha iliyopigwa kwenye Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Tarehe 25 Julai 2022 ikionyesha kuwa moduli ya maabara ya Wentian imetua kwa mafanikio pamoja na muunganisho wa mbele wa moduli ya msingi ya Tianhe. (Xinhua/Guo Zhongzheng) |
BEIJING - Kwa mujibu wa majumuisho ya maendeleo ya majaribio ya utamaduni wa mimea katika kituo cha anga ya juu cha China yaliyotolewa siku ya Jumatatu, mbegu za mimea miwili katika moduli ya maabara ya Wentian ya China kwenye anga ya juu zimeota na sasa ziko katika hali nzuri.
Sampuli za mbegu za mimea hiyo miwili ya Arabidopsis na mpunga, ziliwekwa kwenye kabati ya majaribio ya ikolojia ya maisha ya moduli ya maabara, ambayo ilipelekwa kwenye anga ya juu Mwezi Julai. Majaribio ya kukuza mimea kwenye anga ya juu yalianza Julai 29 huku kukiwa na maagizo kutoka duniani.
“Mbegu za Arabidopsis zimeota majani kadhaa, na miche ya mpunga imekua hadi urefu wa sentimita 30. Baadaye, majaribio yao ya mzunguko wa maisha yatafanywa ili kupata mbegu za anga ya juu,” imesema taarifa ya majumuisho hayo.
“China imefanikiwa kupata mbegu za Arabidopsis za anga ya juu kupitia majaribio yake ya awali ya mzunguko wa maisha angani,” amesema Zheng Huiqiong, mtafiti katika Kituo cha utafiti wa Sayansi ya Mimea ya Molekuli Bora chini ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China.
Zheng ameongeza kusema kuwa majaribio ya mzunguko wa maisha ya mpunga katika moduli ya maabara ya Wentian ya anga ya juu yatafaulu na kutoa mwongozo wa kinadharia wa uzalishaji wa nafaka kwenye anga ya juu.
“Ukuaji wa mimea kwenye anga ya juu unakabiliwa na matatizo kama vile muda wa maua kuchelewa, kiwango kidogo cha kuweka mbegu, na kupungua kwa ubora wa mbegu, na ni mazao machache tu kama vile rape za kuzalisha mafuta, ngano na mbaazi ambayo yamekamilisha majaribio angani ili kupata mbegu,” amesema Zheng.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma