Karakana ya Luban yawa daraja kati ya China na Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2022

Capo-Chichi Segnon John-Isaac Oluwaseyi (kulia), mwanafunzi kutoka Benin ambaye anasoma katika Chuo Kikuu cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia cha Tianjin, akitazama mfano wa mazonge madogo ya panya katika Mashindano ya Ustadi ya Vyuo vikuu vya Ufundi wa Kazi vya Dunia mwezi huu. (Picha na China Daily)

Capo-Chichi Segnon John-Isaac Oluwaseyi, mwanafunzi kutoka Benin anayesoma katika Chuo Kikuu cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia cha Tianjin, alisema kuwa "anajivunia" sana kwa kuwa yeye na timu yake walipata medali ya dhahabu katika mashindano ya ngazi ya kimataifa ya kuongoza panya kutembea ndani ya mazonge.

Wisit Saenklu mwenye umri wa miaka 28 ni mmoja kati ya wahitimu wa kwanza wa Karakana ya Luban nchini Thailand iliyoanzishwa na Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Kazi cha Bohai cha Tianjin ambao ni mradi wa kwanza ulioanzishwa na chuo kikuu kimoja cha China katika ng’ambo.

Saenklue alimwambia mwalimu wake kwamba hivi majuzi amepata kazi mpya katika kampuni ya sehemu alipo, na mshahara wake wa mwezi ni dola za kimarekani 1,160 kutokana na ujuzi na teknolojia alizozipata nchini China. Alisema, kazi yake ya kwanza ni " nzuri na yenye mshahara wa juu kuliko zile walizopata wenzake ".

Watu hao wawili walituonesha uwezekano unaotokana na mipango ya mafunzo ya ufundi wa kazi iliyotolewa na vyuo vya ufundi na teknolojia za kazi nchini China.

Yang Yan, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti na Uenezi cha Karakana ya Luban cha Tianjin alisema kuwa mpaka sasa, Karakana 25 za Luban zilizoanzishwa katika nchi 23 zimekuwa daraja la urafiki kati ya China na nchi na kanda zilizoko kwenye “ Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Vyuo vikuu vya ufundi na teknolojia za kazi vya Tianjin vilikuwa vya kwanza kuanzisha karakana 20 katika nchi 19, karakana 11 zilianzishwa barani Afrika na nyigine zilianzishwa katika nchi za Ulaya na Asia.

Yang alisema kwenye jukwaa la Baraza la kwanza la Maendeleo ya Elimu ya Ufundi wa Kazi Duniani ambalo lilifanyika katika Tianjin kuanzia Agosti 19 hadi 20 kwamba wanafunzi wengi wamekuwa na hamu ya kuendelea na masomo yao nchini China.

Habari zilisema kuwa, kiwango cha mafunzo cha Karakana ya Luban kimesifiwa na watu wengi nje ya nchi, na karakana 11 kati yao zimetambuliwa na wizara za elimu katika nchi washirika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Adolf Mkenda alisema kuwa “Tanzania inakaribisha sana ushirikiano na China katika kuboresha mafunzo ya ufundi wa kazi ili kuongeza nguvu ya uzalishaji na maendeleo ya jamii na uchumi.” 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha