

Lugha Nyingine
Roboti yaweza kupunguza shinikizo ya wahudumu wa kupima virusi
Roboti ikichukua sampuli kwa ajili ya kupima virusi vya korona kwenye Mkutano wa pili wa Roboti wa Dunia 2022 hapa Beijing, Agosti 18. (Picha ilipigwa na Chen Xiaogen/China Daily)
Katika wimbi la joto lililodumu kwa siku nyingi Kusini mwa China, ni changamoto kubwa kwa madaktari waliovaa mavazi mazito ya kujikinga na virusi kuchukua sampuli ya kupima virusi vya korona kwenye vituo vya upimaji vya UVIKO-19.
Hivi sasa, roboti iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Tsinghua na Kampuni ya teknolojia Biotek Corp kwa pamoja, inaweza kuwasaidia madaktari kuepuka joto kali.
Watengenezaji wake walisema, roboti hii inaonekana kama mashine ya kujiendesha ya kuuza vitu, inaweza kuchukua sampuli ya virusi, kupima sampuli, kupata matokeo ya upimaji na kutuma matokeo kwenye intaneti ndani ya dakika 45 bila ya maabara au maingiliano yoyote ya binadamu.
Wataalam wamesema, uvumbuzi huo mpya ni sehemu moja ya majaribio mfululizo ya teknolojia yanayofanywa na kampuni na taasisi za China kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya UVIKO-19, na pia inaonesha maendeleo ya China katika viwanda vya roboti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma