

Lugha Nyingine
Moyo bandia waruhusiwa kuingia soko
(Picha inatoka Chinadaily.)
Moyo bandia uliotengenezwa kwa kuunganisha teknolojia ya roketi na matibabu ya China umepata ruhusa ya kuuzwa sokoni baada ya kupata kibali cha mamlaka ya bidhaa za matibabu ya taifa.
Mfumo wa usaidizi wa moyo HeartCon au “Moyo wa Roketi”, ambao ulitengenezwa na kampuni ya matibabu ya Rocor kwa kujitegemea, ulipata kibali cha kuuzwa sokoni cha Mamlaka ya Usimamizi wa Dawa ya China.
Mtafiti mkuu wa mradi wa majaribio kwenye hospitali, ambaye pia ni mkuu wa Hospitali ya kimataifa ya moyo na mishipa ya TEDA Liu Xiaocheng alisema, “aina hii ya moyo bandia iliyotengenezwa nchini China inatazamiwa kuleta manufaa kwa wagonjwa wenye hali mbaya ya moyo na familia zao humu China.”
Kabla ya HeartCon, aina mbili nyingine za moyo bandia pia zimeruhusiwa na serikali kuuzwa sokoni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma