

Lugha Nyingine
Mashirika ya China yatoa vyombo vya kutumia maji safi kwa shule za kusini mwa Ethiopia
Juni 22, 2022, wanafunzi wa shule ya msingi ya Jimbo la Kusini la Ethiopia wakikunywa maji safi yanayotolewa kwenye chombo cha kutengeneza maji safi kwa teknolojia ya hali ya juu vilivyochangiwa na mashirika ya China. (Xinhua)
Mashirika ya China yametoa vyombo vya kutumia maji safi vinavyohitajika haraka kwa shule za msingi zilizochaguliwa kusini mwa Ethiopia.
Vyombo vitano vya kutengeneza maji safi kwa teknolojia ya hali ya juu vilivyochangiwa pamoja na Kituo cha Maendeleo ya Nguvu ya Uongozi ya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha Qinghua cha China, Kundi la HurRain NanoTech na Mfuko wa Maendeleo ya Vijiji wa China (CFRD) vimefaulu kusambazwa katika shule za msingi za Jimbo la Kusini la Ethiopia, yaani shule za Key-Afer、Tulungo、Sitimba、Turmi na Demeka, ambavyo vitawaletea maji safi wanafunzi 2106 wa shule za msingi za Ethiopia.
Roman Tesfaye, Mke wa Rais wa zamani wa Ethiopia alitoa shukrani za dhati kwa wafadhili na pande zote za kutoa uungaji mkono, akisema kuwa vyombo hivyo vinafaa sana hali ya hewa ya Jimbo la Kusini, watoto wanaweza kupata maji safi bila wasiwasi. Ethiopia inakabiliwa na ukame na ukosefu wa maji, hasa vyombo hivyo vya kutengeneza maji kwa teknolojia ya hali ya juu bila kutoa uchafu na takataka za chupa za plastiki, ambavyo vitaleta manufaa moja kwa moja kwa shule na jamii.
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Demeka Messele Mesfen alifurahi sana baada ya kupokea msaada huo, shule hiyo ambayo ni moja ya shule zilizonufaika, alisoma mara kadhaa maelezo ya matumizi ya vyombo hivyo, na kuahidi kuvitunza vyema vyombo hivyo na kuwawezesha watoto wanufaike ipasavyo. Mkuu huyo alitoa shukrani kwa niaba ya walimu na wanafunzi wote kwa wafadhili wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma