Satelaiti za hali ya hewa za China zilizorushwa hivi karibuni zimeanza kufanya kazi kwa majaribio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2022

Roketi ya Changzheng No. 4 C iliyobeba satelaiti ya Fengyun-3 E (FY-3E) ikirushwa kutoka Kituo cha Urushaji wa Satelaiti cha Jiuquan Kaskazini-Magharibi mwa China, Julai 5, 2021. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)

BEIJING - Jumatatu wiki hii, Idara ya Hali ya Hewa ya China imesema kwamba, satelaiti mbili za hali ya hewa, pamoja na mifumo ya matumizi yake duniani, zilianza kufanya kazi.

Setilaiti hizo mbili, Fengyun-3E na Fengyun-4B, zitatoa data za ufuatiliaji na huduma za matumizi kwa watumiaji wa kimataifa.

Hadi sasa nchi ya China imesharusha satelaiti 19 za Fengyun kwa ujumla, ambazo zinatoa bidhaa na huduma za data kwa nchi na kanda 123 duniani kote huku satelaiti saba zikiwa kwenye obiti kwa sasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha