Kituo cha anga ya juu cha China kuingia kipindi kipya cha matumizi na maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2022

Katika picha hii ya kuunganishwa, wanaanga Zhai Zhigang, Wang Yaping na Ye Guangfu (kutoka kushoto hadi kulia) wakiwa wanatoka nje kutoka kwenye chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-13 kinachorejea duniani katika eneo la kutua huko Dongfeng la Mkoa wa Mongolia ya Ndani nchini China Aprili 16, 2022. (Xinhua)

BEIJING - Kituo cha anga ya juu cha China kitaingia katika kipindi kipya cha matumizi na maendeleo, kipindi hicho kitachukua zaidi ya miaka 10 baada ya kukamilika kwa ujenzi wake mwaka huu, kwa mujibu wa mkutano na waandishi wa habari wa Jana Jumapili.

“Mpango wa hatua ya kwanza ni kurusha vyombo viwili vya kubeba watu kwenye anga ya juu na vingine viwili vya mizigo kila mwaka wakati wa kipindi kipya ” Hao Chun, Mkurugenzi wa Idara ya Anga ya Juu ya China, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Hao amesema kwamba, wanaanga watakaa kwenye obiti kwa muda mrefu, watafanya majaribio ya kisayansi na kiteknolojia ya anga ya juu, na kukarabati kituo cha anga ya juu.

Ili kuboresha zaidi uwezo wa kina na kiwango cha kiteknolojia cha mpango wa anga ya juu wa China, kizazi kipya cha roketi za kubebea na vyombo vya anga ya juu vitatengenezwa, Hao amesema. Roketi za kubebea za kizazi kipya na vifaa vya kutumia kurejea vya chombo kipya cha anga ya juu vitatumika tena.

Chombo cha anga ya juu cha kizazi kipya kitakuwa na uwezo wa kubeba wanaanga saba, na uwezo wake wa kubeba mizigo utaboreshwa sana.

Katika kipindi cha matumizi na maendeleo, majaribio makubwa zaidi ya utafiti wa anga ya juu na majaribio mapya ya teknolojia yatafanywa katika nyanja zinazohusu sayansi ya uhai wa maisha kwenye anga ya juu na utafiti juu ya mwili wa binadamu, sayansi ya fizikia ya nguvu ya mvutano, unajimu wa anga ya juu na sayansi ya Dunia.

Mwaka 2023, China inapanga kuzindua darubini yake kubwa ya kwanza ya kufanya utafiti wa anga ya juu. "Tutafanya utafiti wa kisasa wa kisayansi juu ya uundaji na mageuzi ya muundo wa Ulimwengu, nyenzo na nishati za giza, sayari zinazozunguka mwezi nje ya orbiti na mfumo wa jua, na kutarajia kufikia uvumbuzi kadhaa," Hao amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha