China yapanga malengo ya nishati kwa Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2022

Picha iliyopigwa Desemba 8, 2021 ikionesha mitambo ya kuzalisha umeme kwa upepo katika Shamba la kuvuna Upepo la Changma katika Mji wa Yumen wa Mkoa wa Gansu, Kaskazini Magharibi mwa China.  (Xinhua/Fan Peishen)

Idara ya Nishati ya Taifa ya China imetangaza mwongozo wa maendeleo ya nishati kwa Mwaka 2022, ambao umeeleza ipasavyo malengo ya kuhakikisha ugavi wa nishati na kuongeza ufanisi wa nishati.

Mpaka Mwaka 2022, uwezo wa uzalishaji wa nishati wa mwaka nchini China utafikia tani bilioni 4.41 za makaa sanifu, huku utoaji wa mafuta ghafi utafikia tani milioni 200 hivi.

Mwongozo unasema, inakadiriwa utoaji wa gesi asilia utafikia mita za ujazo bilioni 214.

Na pia unalenga kupunguza kwa utaratibu utegemezi wa nchi kwa makaa ya mawe, ukiahidi kuinua kiwango cha utumiaji wa nishati mbadala mpaka asilimia 17.3 hivi katika matumizi ya nishati ya jumla nchini China.

Mwongozo unasema, nishati inayotokana na upepo na mwanga wa jua itachukua asilimia 12.2 hivi ya matumizi ya nishati ya jumla.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha