Kiongozi wa DPRK Kim Jong Un atoa amri ya majaribio ya kurusha aina mpya ya Makombora ya Masafa Marefu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2022

NEW YORK - Shirika la Habari la DPRK (KCNA) limeripoti mapema leo kwamba jaribio la kurusha aina mpya ya kombora la masafa marefu (ICBM) Hwasongpho-17 la vikosi vya kimkakati vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) limefanyika Jana Alhamisi saa za huko, chini ya mwongozo wa moja kwa moja wa kiongozi wa DPRK Kim Jong Un,

Kwa mujibu wa KCNA, Kim ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha DPRK, Rais wa DPRK na Kamanda Mkuu vikosi vya kijeshi vya DPRK, siku ya Jumatano wiki hii alitoa amri kwa maandishi ya kufanya majaribio ya urushaji wa makombora ya aina mpya ya ICBM ya vikosi vya kimkakati vya DPRK. Alitembelea uwanja wa urushaji wa makombora siku ya Alhamisi wiki hii na akaongoza mchakato mzima wa jaribio hilo la urushaji wa makombora.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha