

Lugha Nyingine
China yapata maendeleo katika utafiti wa chanjo dhidi ya virusi vya Omicron
(Picha inatoka China Daily.)
Ofisa mwandamizi wa China Jumamosi iliyopita katika mkutano na waandishi wa habari alisema, utafiti kuhusu chanjo dhidi ya virusi vya korona aina ya Omicron umepata maendeleo.
Ofisa wa Kamati ya Afya ya Taifa (NHC) Zheng Zhongwei amesema, baadhi ya chanjo zimemaliza utafiti wa kabla ya majaribio ya matibabu, na mchakato wa kuomba ruhusa ya majaribio ya matibabu unaendelea.
“Utafiti umeonesha, virusi vya korona aina ya Omicron havijaepuka kabisa chanjo zilizopo sasa, ” amesema Zheng, akiongeza kuwa udungaji wa chanjo kikamilifu unaendelea kufanya kazi katika kupunguza hatari ya kulazwa hospitali, kuwa mahututi na kutokana na virusi vya Omicron.
Zheng amesema, hivi sasa China ina aina 29 za chanjo ambazo zimeanza kufanyiwa majaribio ya matibabu, na katika chanjo hizo, 16 ziko kwenye kipindi cha III cha kufanyiwa majaribio ya matibabu nje ya China. Ameongeza kuwa, aina 7 za chanjo zimeidhinishwa kuuzwa sokoni kwa masharti au kutumiwa kwa dharura, na aina 2 zimeorodheshwa katika orodha ya matumizi ya dharura ya WHO.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma