China yatoa idhini kwa Vifaa vya kujipima na kugundua virusi vya korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2022

(Picha inatoka ChinaDaily.)

Serikali ya China imeidhinisha vifaa vya aina tano vya kujipima na kugundua virusi vya korona vinavyotengenezwa na kampuni za China kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kupima na kugundua baini mapema ili kukabiliana na virusi vya Korona aina ya Omicron vyenye uwezo zaidi wa kujificha na kuambukiza.

Katika uarifu mbili zilizotolewa Ijumaa na Jumamosi zilizopita, Idara ya Ukaguzi na Usimamizi ya Dawa ya Taifa ya China iliruhusu kampuni tano kurekebisha vyeti vyao vya vifaa vya kupima na kugundua virusi vya korona ili kuruhusu matumizi ya kujipima.

Uidhinishaji huo unatolewa baada ya mfumo wa pamoja wa kukinga na kudhibiti virusi vya korona wa Baraza la Serikali la China kutangaza Ijumaa iliyopita kuwa itaruhusu watu kununua vifaa hivyo vya kujipima katika maduka au kwenye tovuti za mtandao.

Vifaa vya kujipima na kugundua virusi vya korona vinaweza kutumiwa kwa watu wenye homa au dalili nyingine za upumuaji ndani ya siku tano, watu walio karantini na wengine wanaotaka kujipima tu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha