Tanzania yapendekeza kutumia teknolojia ya Juncao ya China ili kukuza kilimo endelevu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2022

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Mashimba Ndaki (wa kwanza kulia) akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya taifa kuhusu "Matumizi ya Teknolojia ya Juncao na Mchango wake katika Mafanikio ya Kilimo Endelevu na Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania" jijini Dar es Salaam, Tanzania, Machi 8, 2022. Serikali ya Tanzania ilipendekeza kuthibitishwa kwa teknolojia ya Juncao ya China ili kukuza kilimo endelevu na sekta ya mifugo katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Juncao, ambayo maana yake halisi ni "uyoga" na "nyasi," kama jina lake linavyoeleza, inaweza kutumika kukuza uyoga wa chakula, chakula cha mifugo au kizuizi cha kijani kuzuia kuenea kwa jangwa. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

DAR ES SALAAM - Serikali ya Tanzania imependekeza kutumia teknolojia ya Juncao ya China ili kukuza kilimo endelevu na sekta ya mifugo katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Juncao, ambayo maana yake halisi ni "uyoga" na "nyasi," kama jina lake linavyoeleza, inaweza kutumika kukuza uyoga wa chakula, kutumika kwa chakula cha mifugo au kizuizi cha kijani katika kuzuia kuenea kwa jangwa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mashimba Ndaki, amesema Serikali imeanza mpango wa kuomba fedha kutoka Serikali ya China kwa ajili ya kutekeleza teknolojia ya Juncao kwa ajili ya lishe ya mifugo na uzalishaji wa uyoga.

Ndaki alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya taifa kuhusu “Matumizi ya Teknolojia ya Juncao na Mchango wake katika Mafanikio ya Kilimo Endelevu na Malengo ya Maendeleo Endelevu nchini Tanzania”. Teknolojia ya Juncao imeendelezwa na Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Uhandisi cha Teknolojia ya Juncao cha Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian (FAFU) cha China.

 “Teknolojia ya Juncao itaongeza uzalishaji na matumizi ya uyoga, jambo ambalo litachangia usalama wa chakula nchini hivyo kufikia Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030 nchini,” Ndaki amesema wakati wa warsha hiyo ya siku nne ambayo imewakutanisha watunga sera wa taifa hilo, wasomi, watafiti, wakulima, wafugaji na wataalam kutoka FAFU na Umoja wa Mataifa (UN).

Amesema teknolojia ya Juncao itachangia ongezeko la upatikanaji wa malisho na kuongeza tija ya mifugo ambayo itasaidia kupunguza umaskini na kuinua pato la taifa.

Lin Zhanxi, mwekezaji wa teknolojia ya Juncao, na mwanasayansi mkuu na mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Uhandisi wa Teknolojia ya Juncao cha Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian (FAFU) cha China, amesema kwenye warsha hiyo kwa njia ya video kwamba, teknolojia ya Juncao inasaidia katika kurekebisha na kupunguza changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Yuan Lin, Mwambata wa Biashara katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, amesema katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, teknolojia hiyo ya Juncao ambayo ni ya muhimu na yenye ufanisi imethibitishwa katika zaidi ya nchi 100 duniani.

"Siyo tu kwamba inasaidia kutengeneza mamia ya maelfu ya nafasi za ajira katika sekta zisizoleta uchafuzi wa mazingira, kuondoa watu kutoka kwenye umaskini na kutambua usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, lakini pia ina jukumu muhimu katika kukuza matumizi ya nishati mbadala na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi," amesema.

John Machiwa, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia ya Uvuvi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema nchini Tanzania kuna wakulima 5,000 wa uyoga wanaozalisha tani 1,000 za uyoga kila mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha