Kampuni kubwa za Teknolojia za China zajitahidi kufikia uwiano wa kaboni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2022

Picha iliyopigwa kutoka angani Mei 24, 2021 ikionesha kituo cha data cha Tencent kilichoko Eneo Jipya la Gui'an, Mkoa wa Guizhou, Kaskazini Magharibi mwa China. (Xinhua/Ou Dongqu)

Kampuni kubwa za teknolojia za China zimekuwa zikifanya juhudi za kupunguza utoaji wa kaboni, kuendana na ahadi ya serikali ya kufikia kilele cha utoaji wa kaboni wa China kabla ya Mwaka 2030, na kuzimua kaboni kabla ya Mwaka 2060.

Utafiti unakadiria kuwa, ifikapo Mwaka 2040, teknolojia ya upashanaji wa habari na mawasiliano ya habari itachukua asilimia 14 ya utoaji wa kaboni wa Dunia nzima, kiwango hicho kikiongezeka kutoka asilimia 1.5 mwaka 2018.

Alhamisi ya wiki iliyopita, Tencent ilitangaza mpango wake wa kuzimua kaboni katika uendeshaji wake na mnyororo wake wa ugavi kabla ya 2030, na pia itatumia nishati isiyochafua mazingira kuzalisha asilimia 100 ya umeme inayoutumia ifikapo 2030.

Lenovo, mtengenezaji mkubwa zaidi wa kompyuta duniani, imevumbua teknolojia ya kupozea kioevu kwenye kituo cha data. Inaweza kupunguza utumiaji wa nishati kwa asilimia 40 huku ikidumisha utendaji wake.

Katika Mkutano wa Dunia wa Simu za kushika mkononi (MWC) 2021 uliofanyika Shanghai, Huawei ilitangaza mtandao wake usiotoa kaboni kabisa, ambao umeundwa kusaidia waendeshaji wa huduma za mawasiliano ya simu kupunguza utumiaji wao wa nishati, kuongeza uzalishaji wa umeme usiochafua mazingira, na kuzimua kaboni katika huduma zao za kila siku.

Pony Ma, Mwenyekiti wa Tencent, amesema kuwa kuzimua kaboni kunaonesha kampuni za teknolojia za kiwango cha juu zinabeba majukumu yao ya kijamii. Umuhimu wa hatua hizo kupunguza zaidi utoaji wa kaboni wa kampuni hizo, ni kuhamasisha kampuni za sayansi na teknolojia kujitahidi kufanya uvumbuzi ili kusukuma mbele mageuzi ya kupunguza utoaji wa kaboni nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha