Kampuni ya kutengeneza simu ya Vivo kutoka China yazindua simu ya kisasa ya 5G nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2022

NAIROBI - Kampuni ya kutengeneza simu za mkononi ya Vivo kutoka China Jumatatu wiki hii imetangaza uzinduzi wa simu ya kisasa ya 5G ya aina ya V23 nchini Kenya.

Shyam Xie, Meneja Mkuu wa Vivo Kenya, amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya kwamba simu hiyo ya kisasa kabisa itapatikana kwa bei ya reja reja ya shilingi za Kenya 59,999 (dola 528 za Marekani).

Amesema Mwaka 2021 kampuni hiyo ilipata mafanikio ya uvumbuzi licha ya mazingira magumu ya kiuchumi.

"Mwaka jana, thamani ya jumla ya mauzo yetu iliongezeka kwa asilimia 230, na kupanua timu yetu kwa mara mbili hadi wafanyakazi 250. Sasa tunafanya kazi na washirika zaidi ya 300 na ninaamini itaendelea kukua katika siku za usoni," amesema.

Amebainisha kuwa Kampuni ya Simu ya Vivo iliingia kwenye soko la Kenya Mwaka 2019 na imekuwa ikipanua shughuli zake nchini Kenya kama sehemu ya mkakati wake wa kuharakisha ukuaji katika masoko mbalimbali duniani.

James Irungu, Meneja wa chapa na Mawasiliano wa Vivo Kenya, amesema kuwa watumiaji wanaohitaji sana, waweka mitindo wanaozingatia mitindo na wapiga picha wanaofanya kazi vizuri wataona simu ya V23 5G inatoa mchanganyiko bora wa umaridadi wa muundo, hali ya juu ya picha na ufanisi bora wa 5G kwa michezo ya simu za mkononi.

Ameeleza kuwa simu hiyo ya V23 5G inatoa uwezo wa kipekee wa kamera katika nyanja mbalimbali za picha za kujipiga zenye ubora wa ajabu na picha za sura ya uso, ikiwa ina ubunifu mzuri na uzani mwepesi, muundo wa kifahari ambao ni wa mtindo lakini wa kuvutia na muonekano wake wa kipekee wa kubadilisha rangi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha