

Lugha Nyingine
Huawei yaisaidia Zambia kuingia kwenye “zama ya 5G”
(CRI Online) Januari 12, 2022
Kampuni ya MTN inayotoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Zambia kwa kushirikiana na Kampuni ya Huawei ya China, imezindua rasmi mtandao wa 5G, na kuifanya Zambia kuwa nchi ya mapema zaidi kuwa na mtandao wa 5G barani Afrika.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Zambia Felix Mutati amesema, mtandao wa 5G ni zawadi ya mwaka mpya kwa wananchi wa Zambia, na kutokana na ushirikiano na kampuni ya Huawei, Zambia imekuwa moja ya nchi kumi za mapema zaidi kuwa mtandao wa 5G barani Afrika.
Hatua hiyo imeboresha zaidi kiwango cha miundombinu ya mawasiliano na upashanaji wa habari nchini humo, na kuweka msingi imara kwa mpango wa kidigitali unaoendelea kutekelezwa.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma