Mtandao wa Treni za Ardhini wa Shanghai waendelea kuongoza kwa urefu zaidi Duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2021

Mafundi wakifanya majaribio ya treni za ardhini katika njia Na. 18 ya treni ya ardhini huko Shanghai Mashariki mwa China, Aprili 26, 2021. (Xinhua/Fang Zhe)

SHANGHAI, China - Huku njia mbili mpya za treni za ardhini zikitarajiwa kuanza kutumika kuanzia leo (Alhamisi) Tarehe 30 Desemba, urefu wa jumla wa mtandao wa treni za ardhini wa Mji wa Shanghai ulioko Mashariki mwa China utaongezeka hadi kufikia kilomita 831, ukiendelea kuwa mrefu zaidi duniani.

Mamlaka ya Usafiri wa Treni za Ardhini ya Shanghai, imeeleza Jumatano wiki hii kwamba, kuzinduliwa kwa njia hizo mbili mpya kutafikisha idadi ya njia za treni za ardhini zinazojiendesha bila dreva hadi tano, zikiwa na urefu wa kilomita 167, hivyo kuifanya Shanghai kuwa ya kwanza duniani kwa mara ya kwanza.

Njia mpya Na. 14 ya treni ya ardhini yenye urefu wa kilomita 38 ndiyo njia ya kwanza inayotumiwa na treni yenye mabehewa manane ya kujiendesha bila dreva mjini Shanghai. Ikiwa na vituo 31, inatarajiwa kuwa njia muhimu ya huduma za treni katika mji huo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha