

Lugha Nyingine
Tanzania kuanzisha maabara za kompyuta shuleni ili kukuza taarifa za kidijitali
DAR ES SALAAM - WAZIRI wa Nchi wa Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wa Tanzania Ummy Mwalimu ametangaza kwamba shule zote mpya za sekondari za umma zitakazojengwa zitawekewa maabara za kompyuta ili kuongeza taarifa za kidijitali katika nchi hiyo.
Ummy Mwalimu amesema kwamba kuundwa kwa maabara za kompyuta katika shule mpya za sekondari za umma kutawawezesha walimu kufundisha teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) somo la msingi la taarifa za kidijitali.
Mwalimu ameyasema hayo Alhamisi ya wiki hii wakati alipofungua mkutano wa siku tatu wa walimu wakuu wa shule za sekondari ulioandaliwa kwa pamoja na Global Education Link (GEL) na Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam.
Mwalimu amesema, serikali inapanga kufungua maabara za kompyuta na vifaa vya TEHAMA kwenye shule mpya 1,500 za sekondari katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mwaka 2022.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma