

Lugha Nyingine
Watafiti wa Israeli wagundua mbinu ya Akili Bandia (AI) inayoweza kuondoa uvimbe wa saratani
JERUSALEM - Watafiti kutoka Chuo cha Huduma ya Afya cha Rambam nchini Israel wamegundua na kufanyia majaribio mbinu ya matibabu ya Akili Bandia (AI) yenye uwezo wa kuondoa uvimbe wa saratani.
Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo kubwa zaidi Kaskazini mwa Israel, mbinu hiyo mpya inashughulikia uvimbe wa saratani ya sakoma, ambayo inajulikana kwa ukinzani wake dhidi ya kemotherapi..
Uvimbe huo hauwezi kuondolewa kwa upasuaji kwa sababu uko karibu na viungo, neva, au mishipa ya damu muhimu.
Ili kukabiliana na uvimbe huu, watafiti wa Rambam wamebuni matibabu ya mionzi yenye nguvu ya juu kupitia gridi ya mtandao au wavu, ili kushambulia uvimbe kwa kuulenga kwa usahihi.
Wameunda mfumo huo wa matibabu kwa kutumia mahesabu magumu ya kiwango cha mionzi, pamoja na Akili Bandia (AI) kuamua njia ya mionzi.
"Tunatumia mionzi sahihi sana, kama kisu cha kupasulia, kwa hivyo matibabu hayana uchungu, na inafanana sana na kipimo cha CT scan" watafiti wameelezea.
Wamejaribu mbinu hiyo kwa wagonjwa watatu wa Israeli, na matokeo yalionesha kuwa uvimbe kwenye miguu yao uliondolewa kabisa bila hitaji la matibabu ya kemotherapi au kukata miguu.
Wamesema kuwa, kutokana na mafanikio ya kesi hizo za kwanza za saratani, inawezekana kupanua matibabu kwa ajili ya aina nyingine za saratani zilizosambaa zaidi mwilini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma