

Lugha Nyingine
Teknolojia za akili bandia yatumiwa katika uendeshaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022
Kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, vifaa hivi vya teknolojia vitawashangaza watazamaji sana!
Mfumo wa kutumia carbon dioxide kuzalisha barafu, ambao utoaji wa kaboni karibu sifuri
Hii ni ndani ya jumba la kitaifa la michezo ya mbio ya kuteleza kwenye barafu. (People’s Daily Online/Hu Xuerong)
Jumba la kitaifa la michezo ya mbio ya kuteleza kwenye barafu linaloitwa “Njia ya Hariri ya Barafu” linazalisha barafu kwa kutumia carbon dioxide, ambayo si kama tu haiharibu tabaka la ozoni bali pia kuwa na ufanisi wa juu zaidi wa kuzalisha barafu. Habari zinasema kuwa utoaji wa kaboni wa mfumo huo unakaribia sifuri, kila mwaka unaweza kuokoa umeme kwa kilowatisaa zaidi ya milioni moja.
Teknolojia ya kupima dawa ya matumzi ya kuongeza nguvu kwa urahisi, kwa kutegemeka, na kwa utulivu
Teknolojia ya kupima dawa ya kuongeza nguvu. Picha inatoka: Idara kuu ya Michezo ya kitaifa
Teknolojia hiyo itakuwa mbinu yenye nguvu katika kugundu wachezaji waliotumia dawa ya kuongeza nguvu na uwezo kwenye mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing 2022.
Vifaa vyenye teknolojia ya 5G+4K/8K vya kutangaza michezo kwa usafi kwenye kiwango cha juu zaidi
Kwa kulinganishwa na mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyofanyika hapo kabla, teknolojia ya hali ya juu inayotumika kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 itaonesha kwa uhalisia hali ya mashindano, ambapo watu wa maeneo mengi zaidi duniani watatazama vizuri michezo hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma